Home Habari za michezo BAADA YA JANA KUMUONGELEA ‘MBOVU’….MAYELE LEO KAJA NA HILI TENA KWA NTIBAZONKIZA..

BAADA YA JANA KUMUONGELEA ‘MBOVU’….MAYELE LEO KAJA NA HILI TENA KWA NTIBAZONKIZA..

Habari za Yanga leo

Baada ya jana kujirekodi video akiwa Instagram huku akimtolea ‘shiti’ mwenzake na timu yake, STRAIKA wa Yanga, Fiston Mayele amempongeza Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ wa Simba kwa kumpa changamoto ya ushindani wa kuwania kiatu cha ufungaji bora dakika za mwisho, huku akitaja sababu zilizopelekea hilo.

Wakati zimesalia mechi mbili za kufunga msimu Mayele alikuwa na mabao 16 na Saido 10 ambapo akabadili upepo mchezo dhidi ya Polisi Tanzania akifunga mabao matano Simba ikifunga mabao 6-1.

Jambo lililomfanya Mayele acheze mechi ya mwisho dhidi ya Prisons waliyokabidhiwa taji, akafunga bao moja kati ya mawili na kufikisha idadi ya mabao 17 sawa na Saido ambaye dhidi ya Coastal Union alifunga mabao mawili.

Amefafanua hilo “Mechi za Ligi Kuu ziliingiliana na majukumu yangu ya timu ya taifa ndio maana nilisimama muda mrefu bila kufunga, nikiri kwamba Saido kanipa changamoto dakika za mwishoni kabisa.

“Saido ni mchezaji mzuri sana, nilikuwa naye Yanga nimeona uwezo wake, alienda Geita Gold akaonyesha uwezo, sasa yupo Simba bado anafanya vizuri, ninaloweza kumshauri aendelee hivyo hivyo hadi msimu ujao.”

Nje na hilo, amezungumzia alikuwa na msimu mzuri sana, ambao hatakaa ausahau kwenye karia yake ya soka, huku akijivunia kuvunja rekodi ya mabao aliyoyaandika msimu uliopita.

“Siyo jambo jepesi mchezaji kuvunja rekodi yake, nashukuru nimeivunja na kuzidisha bao moja.”
mwisho

SOMA NA HII  HII HAPA TAARIFA MPYA KUHUSU VYUMA VINGINE VITAKAVYOSHUKA SIMBA....