Home Habari za michezo BAJETI YANGA …PESA ZA WADHAMINI WENGINE HAZIONEKANIKI…INJINIA HERSI AJIKANYAGA HADHARANI…

BAJETI YANGA …PESA ZA WADHAMINI WENGINE HAZIONEKANIKI…INJINIA HERSI AJIKANYAGA HADHARANI…

Habari za Yanga

Rais wa Yanga ndugu Hersi wakati anatoa hutuba yake aliweza kusema Yanga imeweza kutengeneza Kiasi cha 7,068,127,083 Kwa mwaka huu wa 2022-2023 kupitia Wadhamini wao ambao ni Sportspesa, Azamtv, GSM, Haier, Jembe Energy, Crdb bank, Unicef, Smile na Robbialac.

Baadae hapohapo Mkurugenzi wa Fedha wa Yanga Sabri Sadick alisoma mapato na Matumizi akionyesha Wadhamini wameweza kuingiza kiasi cha 8,111,663,497.

Hapa tu utaona ni vipi mambo yanavyojichanganya kama mseto kila mmoja anasema namba zake waliosoma CUBA tayari wataelewa.

Lakini Tukumbuke kuwa kuna mikataba imesainiwa na Yanga katika kipindi mwaka wa fedha huu ambayo ni wadhamini namba zake zilizosomwa wakati wa kutangazwa haziendani na zilizosomwa leo:

Mfano hai hii mikataba miwili tu imeweza kufikisha fedha 7B alizosoma Rais wa Yanga bila kuweka wadhamini wengine

08 July 2021 Azam Media ilisaini Mkataba na Yanga wenye thamani ya 41B kwa kipindi cha miaka 10 na kufanya kila mwaka kuchukua 3B.

27 July 2022 Sportspesa wamesaini na Yanga mkataba wa 12.3B kwa kipindi cha miaka Mitatu na kufanya kila mwaka kuchukua 4B

Kwa Maana rahisi mikataba yote mingine Fedha zake hazijajumlishwa au kulipwa kwa Yanga mfano ni hii mikataba miwili toka Makampuni ya GSM yenye jumla kwa mwaka zaidi ya 3.3B haipo kwenye Hesabu za Rais wala za Mkurugenzi wa Fedha ni Hewa.

12 September 2022 GSM walisaini mikataba miwili na Yanga wenye thamani ya 11B kwa kipindi cha miaka Mitano.

Mkataba wa kwanza wa Jezi kwa mwaka 1.5b  na mwingine wa Matangazo ya nembo za GSM kwa mwaka 300m na unaongezeka kila mwaka 10% kwa muda wa miaka Mitano unafanya jumla kuwa fedha 11B.

30/01/2023 Kampuni ya HAIER imesaini mkataba na Yanga wenye thamani ya kiasi cha 1.5b.

Katika Eneo lingine ni namba za MKOPO hapa Yanga imeambiwa imekopeshwa 4,813,675,379 (4.8B)  hii Deni halionyeshi lilianza lini na kwa Vikao gani kuidhinisha ila pia limekwenda katika Maeneo gani?

Sasa Unaomyeshaje Unadai wakati  unadaiwa Fedha za Udhamini wakati huohuo?

Kifupi ni kwamba Ukichukua Matumizi ya Motisha kwa wachezaji na Benchi 2.9b na gharama za maandalizi ya mechi 1.4b na Usajili 2.4 unapata 6.7B haya yote ni Maeneo ambayo Mfadhili alikuwa anasema anatoa fedha zake kumbe Deni limerudi kwa Yanga Tena kwa kiasi anachojua yeye pekee maana Matumizi anapanga yeye.

Kwa nadharia ukipiga hesabu zote halafu ukageukia Mauzo ya Jezi utaona Faida inayopatikana Katika Jezi kdio hiyohiyo inayotumika katika mambo mengine yote na bado hesabu hiyohiyo iliyotumika ndio inaonyeshwa kama ni MKOPO, hii ni sawa na mwizi kukuibia nguo zao wakati unaoga mtoni nae unatoka ikiwa uchi unamkimbiza Utake Usitake wewe ndio Chizi zaidi.

@MtiMkavu

SOMA NA HII  JUMATANO YA MAOKOTO YA MERIDIANBET IMEKUJA NA UHAKIKA WA ODDS HIZI ZA USHINDI...

3 COMMENTS

  1. nadhani upo sawa si vibaya kuhoji kwa undani maana hizi report zinz mapungufu,naomba twende kwa Simba maana wewe unajua sana anza na budget yao na tena utupe status ya Mo na hisa zake na proof ya kuwa Mo ana miliki share 49% na tena utwambie ahakuwaje na hao member huku ajalipa pesa,KIJANA ENGINIA ATAWAPASUA KICHWA USIMBA NA UZUZU WENU HAUTAISHA,timu inaendeshwa kwa kufadhiliwa eti ina mwekezaji na TRY AGAIN juzi alisema simba inahitaji pesa ,muda wa kujitegemea umefika na Mo ni mdhamini HUKUSIKIA siku ya uzinduzi wa sandaland