Home Habari za michezo TAKWIMU ZINAONGEA….YANGA WAMEINGIZA PESA NYINGI KULIKO KLABU ZOTE ZA KENYA KWA UJUMLA...

TAKWIMU ZINAONGEA….YANGA WAMEINGIZA PESA NYINGI KULIKO KLABU ZOTE ZA KENYA KWA UJUMLA WAKE…

Habari za Yanga leo

Mtandao maarufa wa michezo Pulse Soorts umeandika kuwa, klabu ya Yanga imeingiza pesa nyingi msimu wa 2022/23 kuliko klabu zote za kenya kwa pamoja.

Hii imekuja baada ya Yanga kupitia mkutano wake mkuu kutangaza kuwa kwa msimu uliopita, klabu hiyo imeingiza kiasi cha Tsh bilioni 7 huku ikitengeneza faida ya Tsh milioni 500.

Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe ameipost habari hiyo kisha akaandika; “Klabu ya Yanga imeingiza pesa nyinngi kuliko klabu zote za Kenya. Tunaposema KLABU KUBWA tunamaanisha kwa ukubwa huu.

“Makolo walivyo na wivu usishangae WAKAPIKA ubwabwa mwingine na kudanganya watu kuwa wamepata hela nyingi kuliko timu zote za Buza.

“Na wakimuona na jezi namba (6) anayekuja, WATAPIKA ubwabwa mwingine wakutane kuongeza bajeti. Subirini mtakuja kuniambia,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AWASOMA WYDAD AC...AWAINGIZA KWENYE MTEGO HUU HATARI