Home Habari za michezo MASTAA WAPYA SIMBA WAANIKWA …AHMED ALLY ATAJA VYUMA VYA KAZI HASWA…

MASTAA WAPYA SIMBA WAANIKWA …AHMED ALLY ATAJA VYUMA VYA KAZI HASWA…

Habari za Simba leo

Uongozi wa Simba SC umeonesha kuwa makini sana katika kukijenga kikosi chao kwa msimu ujao, hiyo ni baada ya kuweka wazi kwamba utashusha vyuma vya kazi kwa ajili ya kupambania malengo kwa msimu mpya wa 2023/24.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, ipo kwenye mwendelezo wa maboresho ya kikosi chao ikianza kuwapitishia Panga mastaa waliofikia makubaliano ya kutoendelea nao.

Miongoni mwa nyota ambao wamepewa mkono wa asante ni Erasto Nyoni, Beno Kakolanya, Victor Akpan, Nelson Ókwa, Agustine Okrah, Mohamed Ouattara na Jonas Mkude.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuwa mpango mkubwa ni kusajili wachezaji wazuri ambao wataleta ushindani ndani ya kikosi hicho.

“Tutawatambulisha wachezaji wa kazi kwa ajili ya kutupa furaha Wanasimba, unajua hatukuwa na mwendo mzuri msimu ambao umeisha kwa kushindwa kufikia malego kwa asilimia kubwa.

“Msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa, na sisi tunalijua hilo, tunaanza na maboresho kwenye kikosi chetu, kikubwa mashabiki wawe na subira mambo mazuri yanakuja na tutafanya kazi kuwa na timu imara,” amesema Ally.

SOMA NA HII  AL AHLY WAENDELEZA UBABE AFRIKA...WATINGA NUSU FAINALI KLABU BINGWA KWA KISHINDO...