Home Habari za michezo BREAKING NEWS…SIMBA NA YANGA KUPIGWA OKT 19…BODI YA LIGI YATANGAZA

BREAKING NEWS…SIMBA NA YANGA KUPIGWA OKT 19…BODI YA LIGI YATANGAZA

Habari za Simba na Yanga

HATIMAYE Bodi ya Ligi wametangaza Ratiba ya Msimu wa Ligi Kuu 2024/25 ambayo itaanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 16 kwa mchezo mmoja pekee, huku Simba wakifungua Ligi tarehe 18 dhidi ya Tabaora Utd.

Simba SC watafungua msimu wao pale KMC Complex, ambapo inaelezwa kuwa wamechagua kutumia uwanja wa KMC Complex pale Mwenge kwa michezo yake ya nyumbani , lakini mechi kubwa zote zitapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bingwa Mtetezi wa Ligi kuu ya NBC Yanga SC, wataanza kuusaka Ubingwa wa 4 mfululizo kule mkoani Kagera katika Dimba la Kaitaba, kisha watarejea Azam Complex ambapo watapatumia kama Uwanja wa nyumbani pia kwa msimu huu kwa sehemu kubwa ya mechi zao.

Azam FC wao wataanzia kwa Mej.Jen. Isamhuyo vs JKT Tanzania.

MECHI 10 ZA AWALI ZA SIMBA SC 2024/25

Simba vs Tabora Utd
Simba vs Fountain Gate
Tz Prisons vs Simba
Azam FC vs Simba
Simba vs Namungo
Dodoma Jiji vs Simba
Simba vs Coastal Union
Simba vs Yanga Okt 19
Mashujaa FC vs Simba
Simba vs JKT Tanzania.

MECHI 10 ZA AWALI ZA YANGA SC 2024/25

Kagera Sugar vs Yanga
KenGold FC vs Yanga
Yanga vs JKT Tanzania
Yanga vs Mashujaa FC
Singida BS vs Yanga
Yanga vs KMC FC.
Yanga vs Pamba Jiji
Simba vs Yanga
Yanga vs Tabora Utd
Coastal Union vs Yanga

Mechi kubwa inayotazamwa na wengi ni ya Simba na Yanga ambayo itapigwa Oktoba 19, ikiwa ni mechi ya 8 tangu kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC.

SOMA NA HII  AHMED ALLY...KAMA TUSIPOFUZU MAKUNDI UBAYA UBWELA UTATURUDIA