Michezo

SINGIDA FOUNTAIN GATE YABADILI GIA ANGANI

Staff Desk July 7, 2023 2:07 pm

KLABU ya Singida Fountain Gate imefanya mabadiliko ya kambi yake ya mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa mashindano.

Awali klabu hiyo ilipanga kuweka kambi Tunisia.

“Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wa Singida Fountain Gate FC kwamba maandalizi ya msimu ujao kwa klabu yetu yatafanyikia jijini Arusha kuanzia Julai 10, 2023,”imesema taarifa ya timu hiyo.

Kwa mujibu klabu hiyo mabadiliko hayo yanatokana na ufinyu wa muda na kuchelewa kukamilika kwa usajili wa wachezaji, hivyo kulazimika kubaki nchini ili wachezaji wote waweze kushiriki maandalizi hayo kwa wakati.

KWA TAARIFA YAKO SIMBA WAMESHAMPA THAN YOU KIYOMBO….MUDA WOWOTE ANATUA KATIKA KLABU HII KIVUMBI LEO TWIGA STARS KUKIWASHA DHIDI YA CRESTED CRANES

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply