Habari za SImba SC
Habari za michezo

CHAMA HAAMINI MACHO YAKE, UONGOZI WA SIMBA WAMFANYIA UMAFIA

Staff Desk July 15, 2023 12:16 pm

Wakati kiungo Clatous Chama akiitingisha klabu yake, mabosi wake wamecheza mchezo wa kimafia wakimzidi akili kwa kufanya maamuzi ambayo yamemuacha hoi.

Chama alitingisha kutaka kutimka klabuni hapo akitaka kuvunja mkataba na klabu hiyo baada ya kile alichodai mkataba wake uko ukingoni na tayari ameshapata timu.

Hata hivyo mabosi wa Simba walishajua anachotaka kiungo wao huyo na haraka wakaingiza fedha zake zilizobaki za ada ya usajili ambazo zilikuwa zimesalia.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba Chama alitakiwa kulipwa fedha hizo kabla ya msimu ujao kuanza ambapo haraka wakaingiza fedha hizo Julai 13 kwenye akaunti yake.

Kuingizwa kwa fedha hizo kumemuacha njia panda Chama kuendelea na msimamo wake kwa kuwa tayari Simba imeshakamilisha makubaliano yao ya kimkataba.

“Atuambie yeye sasa anataka kwenda lini Uturuki kuendelea na kazi, tunajua alichotaka kufanya na kitu gani alitaka kukitumia, Chama anataka fedha na tayari tumeshamuingizia hizo fedha zake, mkataba unasema alitakiwa kupewa kabla ya msimu mpya kuanza.

Sakata hilo liliwaweka Yanga katika mkao wa kula wakisubiri hatma ya sakata hilo ambapo Mwanaspoti linafahamu kuwa tayari mabosi wa Yanga walishampigia simu wakimuandalia mkataba kwa sharti la kumalizana kwanza na klabu yake.

SIMBA BAADA YA KUMPA THANK YOU SAWADOGO, MAPYA YAIBUKA SIRI YA DUCHU KUREJEA SIMBA YATAJWA, MWENDA KAPOMBE WAHUSISHWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply