Home Habari za michezo BAADA YA KUTOKA YANGA, HUYO MEYELE KAMA MFALME MCHEKI HAPA

BAADA YA KUTOKA YANGA, HUYO MEYELE KAMA MFALME MCHEKI HAPA

Habari za Michezo

Mshambuliaji Fiston ametangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Pyramid FC inayoshiriki Ligi Kuu Misri kutoka klabu ya Yanga ya Tanzania.

Mayele anaondoka Young Africans SC baada ya kuwatumikia Wananchi kwa misimu miwili huku akimaliza nafasi ya pili kwenye kinyang’anyiro cha ufungaji bora kwenye msimu wake wa kwanza, 2021/2022 kabla ya kushinda kiatu cha mfungaji bora (magoli 17) kwenye msimu wake wa pili wa 2022/2023 sambamba na kuibuka mchezaji bora wa msimu (MVP) wa Ligi Kuu Tanzania.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 akiwa Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza na magoli 7.

SOMA NA HII  HIKI KIKOSI CHA SASA TAIFA STARS SIO POA

1 COMMENT