Home Habari za michezo ‘BEKI LA CHAN’ NA YANGA NI SUALA LA MUDA TU….MWENYEWE AANIKA A-Z...

‘BEKI LA CHAN’ NA YANGA NI SUALA LA MUDA TU….MWENYEWE AANIKA A-Z ISHU ILIVYOPIGWA..

Habari za Simba na Yanga

NI suala la muda tu, lakini ukweli ni kwamba beki wa kati wa kimataifa wa Yanga kutoka Mali, aliyekiwasha kwenye fainali za CHAN 2022, Mamadou Doumbia wakati wowote atapewa ‘Thank You’ na klabu hiyo kutokana na kumalizana na klabu hiyo inayoingia sokoni kusaka mbadala wake.

Doumbia aliyesajiliwa dirisha dogo akichomolewa kwenye fainali za CHAN zilizofanyika Algeria, Januari mwaka huu, kuchukua nafasi ya Gael Bigirimana, lakini ameshindwa kupenya kikosini mbele ya nahodha Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimesema kuwa wamefanya uamuzi wa kuvunja mkataba na Doumbia ili kutafuta mchezaji atakayetoa nafasi ya kuwapumzisha wachezaji wengine wanaotumika kwa muda hasa msimu huu kikosi kilipokuwa chini ya Nasreddine Nabi.

“Yanga imefanya kazi kubwa sana msimu huu imetwaa mataji mawili ya mashindano ligi na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kufika hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika hivyo wachezaji wametumika sana wanahitaji mapumziko kwa kuwaongezea watru wa kazi;

“Doumbia sio mchezaji mbaya lakini alishindwa kuingia kwenye mfumo kutokana na kukutana na wachezaji ambao tayari wameonyesha kazi nzuri na timu inahitaji matokeo hivyo hakukuwa na nafasi ya yeye kupewa muda wa kuonyesha.” kilisema chanzo hicho.

Beki huyo aliyesajiliwa kutoka klabu ya Stade Malien ya Mali tangu atue Yanga amecheza dakika 45 katika mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Rhino Rangers, mchezo uliopigwa Januari 29 na watetezi hao wa taji hilo wakishinda mabao 7-0 Kwa Mkapa na Mechi ya Ligi dhidi ya Mbeya City alicheza dakika zote 90.

Alipotafutwa  Doumbia ambaye alikana taarifa hizo aliweka wazi kuwa hajafanya mazungumzo yoyote na uongozi wake labda kama wamemalizana na meneja wake.

“Tangu ligi imemalizika sijazungumza na kiongozi yeyote wa Yanga kuhusu kuvunja mkataba labda nipe muda niongee na meneja kama kuna taarifa hiyo,” alisema Doumbia

Alipoulizwa kama kwa upande wake yupo tayari kubaki Yanga alisema ni mapema sana kuzungumza suala la kubaki au kuto kubaki wakati bado ajakaa na meneja wake kufahamu nini kinafuata baada ya kuanza vibaya ndani ya Yanga mara baada ya kupata mkataba.

Doumbia alifunguka; “Wakati mwingine soka ni katili sana, nimecheza michuano mikubwa na yenye ushindani wa juu, lakini nimekuja huku sichezi, hilo haliwezi kuondoa kwenye malengo na maisha yangu ya soka. Najua katika soka changamoto ni kawaida, ila inahitaji moyo wa ujasiri na kutokata tamaa kwani kila jambo lina wakati, ninachojua mimi ni beki mzuri ukifika wakati wangu nitacheza na watu wananiona.”

Doumbia atakuwa ni mchezaji wa sita kupewa mkono wa kwaheri baada ya Bernard Morrison, Erick Johora, Tuisila Kisinda, Dickson Ambundo na Abdallah Shaibu ‘Ninja’, huku Feisal Salum ‘Fei Toto’ akinunuliwa mapema na Azam kutoka kikosi hicho cha Vijana wa Jangwani.

SOMA NA HII  HIZI HAPA SABABU ZA YANGA KUWA JUU YA MAMELOD SUNDOWNS KWENYE VIWANGO VYA SOKA..