Home Habari za michezo BAADA YA KUTEMWA SIMBA….GADIEL MICHAEL KUENDA HUKU KUPIGA PESA….

BAADA YA KUTEMWA SIMBA….GADIEL MICHAEL KUENDA HUKU KUPIGA PESA….

Tetesi za Usajili Simba

Baada ya kutemwa na Simba, mlinzi wa kushoto Gadiel Michael, yuko mbioni kujiunga na klabu ya Singida Fountain Gate Fc ya mkoani Singida.

Gadiel alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa misimu minne, mabosi wa Simba wakaachana nae baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu.

Singida Fountain Gate pia inatajwa kumsajili mlinda lango Beno Kakolanya ambaye pia ameachwa na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Matajiri hao wa Singida pia wanatajwa kumuwania beki Kennedy Juma ambaye hata hivyo Simba haina mpango wa kumuacha kwa kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja

Zipo taarifa kuwa Kennedy kama ilivyo kwa Joash Onyango, nae aliomba kuachwa ili akajiunge na timu ambayo itampa uhakika wa kucheza.

Kennedy ni miongoni nmwa wachezaji ambao Kocha Robertinho Oliveira alipendekeza kuendelea nao.

SOMA NA HII  ISHU YA SIMBA KUPELEKWA MAHAKAMANI IPO HIVI, MAWAKILI KAMA WOTE WAANDALIWA