Home Habari za michezo KOCHA WA SIMBA ROBERTINHO AFUNGUKA JAMBO ZITO KUHUSU SAFU YA ULINZI SIMBA

KOCHA WA SIMBA ROBERTINHO AFUNGUKA JAMBO ZITO KUHUSU SAFU YA ULINZI SIMBA

Habari za Simba SC

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameweka wazi kwamba kwenye wakati huu wa maandalizi ya msimu mpya (Pre Season) anataka kuhakikisha anatafuta njia mbadala ya kutoruhusu mabao kwenye safu yake ya ulinzi.

Simba msimu uliopita ndio ilikuwa timu iliyoruhusu mabao machache (17) katika Ligi Kuu huku ikiwa kinara kwenye ufungaji ikifunga jumla ya mabao 75.

Licha ya kuruhusu mabao hayo machache, kocha Robertinho ameonyesha wazi bado ana kazi ya kufanya kuhakikisha msimu ujao wanaepuka kabisa kufungwa mabao kiwepesi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Robertinho alisema kwenye kikosi chake anatafuta mzani sawa wa kuwa na wachezaji wakongwe na vijana ili kuhakikisha wanalinda mipira inayopotezwa.

“Upande wa ulinzi ni lazima siku zote uweze kuulinda mpira unaopotea usipotee, mpira wa sasa unahitaji spidi na umiliki mkubwa wa mpira;

“Ukiweza kuumiliki mpira inakufanya uwe na wakati mzuri wa kufanya maamuzi wapi na wakati gani uutoe.”
Robertinho alisema licha ya kuhitaji ulinzi wa kuhakikisha mipira haipotei, siri kubwa ya mpira ni kufungwa kwa mabao mengi kila nafasi inapopatikana.

“Tunahitaji wachezaji ambao wanapenda kufunga kwa sababu siri ya mpira ni kufunga, pia kwenye timu kama Simba inahitaji wachezaji wenye viwango vinavyofanana;

“Ukiwa na wachezaji wazuri wawili kwenye kila eneo kama itawezekana itakuwa nzuri, kumbuka msimu uliopita nikiwa na Simba sijapoteza mechi yoyote na nimeshinda dabi.”

Katika hayo ni wazi mabosi wa Simba wanaendana na kauli ya Robaertinho kwani hadi sasa tayari wameshaimalisha kwenye eneo la ulinzi na ushambuliaji.

Eneo la ulinzi wamewasajili David Kameta na Che Malone huku wakiwaongezea mikataba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomari Kapombe na upande wa washambuliaji yupo Willy Onana na Aubin Kramo.

SOMA NA HII  ALIYMBEBA MAYELE ATAKIWA HUKU