Home Habari za michezo SIMBA WATAMBA KWA USAJILI WAKE HUU, UKUTA UNAOTENGENEZWA NI BALAA

SIMBA WATAMBA KWA USAJILI WAKE HUU, UKUTA UNAOTENGENEZWA NI BALAA

BADO vurugu za usajili zinaendelea katika dirisha hili kubwa la usajili, kwa timu shiriki za Ligi Kuu Bara kila moja ikiboresha kikosi chake ili kifanye vema katika msimu ujao ikiwemo kubeba Kombe hilo.

Wakati usajili huo ukiendelea, Simba tayari imetangaza kuwasajili wachezaji wanne hadi hivi sasa ambao ni mabeki Fondoh Che Malone, David Kameta ‘Duchu’ viungo Aubin Kramo na Willy Onana.

Simba imepania kufanya makubwa katika msimu ujao ikiwemo kuwapoka watani wao wa jadi, Yanga mataji matatu waliyoyachukua kwa misimu miwili mfululizo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la FA pamoja na kufika hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kati ya nafasi ambayo wameonekana Simba kuitolea macho kwa kufanya usajili mkubwa ni nafasi ya ulinzi ambayo hadi hivi sasa wamefanikiwa kumsajili beki wa Cotton Sports ya nchini Cameroon, Fondoh Che Malone na David Kameta kutoka Mtibwa Sugar.

Championi Jumatano linakuletea ukuta wa Simba utakavyokuwa katika msimu ujao huku kukiwa na maingizo hayo mapya ya mabeki ambao itakuwa hivi;

CHE MALONE & INONGA

Hiyo ndio pacha mpya inayotarajiwa kuonekana uwanjani ikicheza pamoja katika safu ya ulinzi eneo la kati itaongozwa na beki bora wa kati wa msimu wa 2021-22, Mkongomani Hennock Inonga atakayecheza pamoja na Che Malone.

Che Malone alisajiliwa kwa dau la Sh 220 Mil akitokea Cotton Sports moja kwa moja ataingia katika kikosi cha kwanza bila ya kuzuiwa na mabeki wengine waliokuwepo hapo.

Ujio wa Che Malone unakuja kusuka ukuta imara katika msimu ujao na yeye amekuja kuchukua nafasi ya Mkenya, Joash Onyango atakayekuwa Singida Fountain Gate.

Che Malone na Inonga hawatachukua muda mrefu kutengeneza kombinesheni ya ushindani katika timu, kutokana na uzoefu, uwezo wa kila mmoja hivyo itachukua muda mfupi kuzoeana, basi tarajia kuona ukuta bora na imara wa Simba katika msimu ujao.

Mbadala wa Che Malone anatarajiwa kuwa Kennedy Juma kama ikitokea amepata majeraha au adhabu ya kadi katika michezo inayofuatia.

KAPOMBE & TSHABALALA

Ni kati ya wachezaji walioongezewa mikataba mipya ya kuendelea kubakia hapo, kwa kila mmoja kusaini miaka miwili itakayomalizika 2025.

SOMA NA HII  VITA YA NAMBA HUKO YANGA SASA IMESHAKUWA MAJANGA...... WAZAWA WAGOMA