Home Habari za michezo WAKATI SIMBA NA AZAM WAKISHUSHA VIFAA VYAO…ENG HERSI KATIKISHA KICHWA KISHA AKASEMA...

WAKATI SIMBA NA AZAM WAKISHUSHA VIFAA VYAO…ENG HERSI KATIKISHA KICHWA KISHA AKASEMA HAYA…

Habari za Yanga

Wakati vilabu vya Simba, Azam FC na Singida wakiendelea kutangaza sajili zao kila kunapokucha.

Hali ni tofauti kwa Klabu ya Yanga ambao mpaka sasa wamemtangaza mchezaji mmoja tu kujiunga na Klabu hiyo, tena mzawa Nickson Kibabage kutoka Singida FG.

Mashabiki wa Yanga wanaonekana kuwa na wasiwasi huku ikizingatiwa Klabu hiyo imeachana na nyota wake kadhaa.

Sasa Rais wa Klabu ya Yanga Injinia Hersi Said ametoka hadharani na kuwapa matumaini Wananchi na kuwapa neno la Matumaini.

Akizungumza Hersi amesema;

“Naona watu wanaposti sajili zao na kutamba mitandaoni wanayanga wasitishike kwani wanayoyafanya sisi tulishayafanya na tutayafanya kwasababu tumesajili na tuna imani na usajili tulioufanya;

“Kwa namna tulivyopata mafanikio Yanga kwenye mashindano ya ndani na kimataifa msimu huu tunahitaji jitihada zaidi ili kuvuka hatua hiyo na kufikia huko tunahitaji uwekezaji kwenye usajili,”

SOMA NA HII  BAADA YA MANENO MANENO KUWA MENGI KUHUSU MKATABA WA KOCHA MPYA..SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI...