Habari za Yanga
Habari za michezo

YANGA WATUA TANGA, KUTETEA NGAO YA JAMII, GAMONDI APATA MTIHANI MZITO

Staff Desk August 8, 2023 6:59 am

Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Tanga kushiriki mashindano ya Ngao ya Jamii Yanga ikitarajiwa kucheza na Azam Fc katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali siku ya Jumatano

Yanga imeondoka jijini Dar es salaam ikiwa na kikosi chake kamili ambapo Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Miguel Gamondi, atatumia mechi za Ngao ya Jamii kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc

Mechi ya mkondo wa kwanza ambayo Yanga itakuwa ugenini inatarajiwa kupigwa August 20 ambapo huenda mchezo huo ukapigwa nchini Tanzania

Timu hizo zitarudiana wiki moja baadae katika mchezo wa pili ambao Yanga itakuwa mwenyeji

Yanga inakwenda Tanga ikiwa na dhamira moja, kutetea Ngao ya Jamii ambayo wametwaa katika misimu yote miwili iliyopita

KELELE ZENU MWISHO NOVEMBA, SIMBA YAANZIA MANUNGU YABAKI UHURU, YANGA YENYEWE YAKIMBILIA AZAM COMPEX HAFIZ KONKONI AMFANYIA UMAFIA BIRIGIMANA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply