Home Habari za michezo KUELEKEA MICHUANO MIPYA YA CAF….MPANGO WA SIMBA MPAKA SASA UMELALIA HAPA…..

KUELEKEA MICHUANO MIPYA YA CAF….MPANGO WA SIMBA MPAKA SASA UMELALIA HAPA…..

Kikosi cha Simba Msimu huu 23/24

MABOSI wa Simba wameweka mikakati ya kufanya vizuri kuelekea michuano ya Super League wanaheshimisha Taifa kwa kufanya vizuri katika michuano hiyo ambayo watakuwa wenyeji.

Simba watakuwa wenyeji wa michuano hiyo ambayo inatarajia kufanyika hapa nchini kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambao uko kwenye ukarabati baada ya Mkandarasi kuanza kufanya ujezi huo.

Katika michuano hiyo ambayo yatashirikisha timu nane kundi la kwanza litakuwa na timu za

Al Ahly ya Misri, Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Wydad Athelic (Morocco), Esperance de Tunis (Tunisia).

Kundi la pili ni TP Mazembe (DR Congo), Petro Luanda (Angola) na Horoya Athelic ( Guinea) na Simba ambao ni wenyeji wa michuano hiyo ambayo ni timu pekee kwa Afrika Mashariki kushiriki michuano hiyo.

Simba wametoa kauli hiyo kufuatia kupokea maofisa wa Shirikisho la Soka Afrika CAF ambao wapo nchini kwa ajili ya ukaguzi wa maandalizi ya michuano hiyo inayotarajia kuanza Oktoba mwaka huu kwa ufunguzi wake kufanyikia kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Gain’ alisema kuwa mikakati yao mikubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri bila ya kuangalia watakutana na wapinzani wa aina gani katika michuano hiyo.

Alisema maandalizi ya michuano hiyo mikubwa yameshaanza kwa sababu walipokea wageni mbalimbali ambao ni maofisa wa CAF kwa ajili ya ukaguzi na maandalizi ya ufunguzi wa mashindano yenyewe ambayo yatazinduliwa hapa nchini.

“Tumekuwa na wakati mzuri wa kujadili na maofisa wa CAF kuelekea maandalizi ya michezo ya Afrika (Afrika Football League) Tanzania tumekuwa wenyeji tukiwakilishwa na kikosi chetu pekee , ndio tunashiriki na tunajiandaa kufanya vizuri

Binafsi kwetu hili ni jambo kubwa kwa kupata nafasi ya kushiriki katika michuano hii mikubwa, malengo yetu ni kuona tunafika mbali kwa timu kuweza kupata matokeo mazuri katika kila mchezo bila ya kujali tunakutana na mpinzani wa aina gani kwa sababu uzoefu wetu ni mkubwa katika soka la Afrika, ” alisema Try Again.

SOMA NA HII  RAGE AIBUKIA YANGA....AMWAGA SIFA KAMA ZOTE..."WANACHOKIFANYA HUWEZI KUKIONA POPOTE PALE:...