Home Azam FC AFADHALI YA ROBERTINHO, SIO HUKO KWA GAMONDI NA HILI LA DABO SASA

AFADHALI YA ROBERTINHO, SIO HUKO KWA GAMONDI NA HILI LA DABO SASA

Tetesi za Usajili Simba

Achana na Robertinho yeye tayari ameshapata mwanga‼️Lakini vipi hawa wawili, Miguel Gamondi wa upande wa Yanga SC pamoja na Youssouph Dabo wa Azam FC wote hawa ni wageni hasa kwenye NBC PL na soka tu kiujumla hapa Tanzania.

Licha ya nature ya aina ya timu zetu na aina ya soka lakini still unaamini kwenye kipindi hiki (MUDA HUU) wanaendelea kuandaa vikosi vyao kuelekea msimu mpya.

Pre-Season huenda imewapa vision ya msimu na mashindano yote watakayoshiriki kwa ujumla. Kisha, hii Ngao ya jamii itawapa sasa mwangaza wa kuelekea NBC PL

Kitu pekee ambacho naweza kuwa upande wao ni ukubwa wa vikosi vyao, lakini pia quality ya hao wachezaji sio yenye wasiwasi sana (kwa wengi wao tuliowaona).

Na ndiyo maana nasema ‘BADO MALI IMFUKONI’, yes, kwakua naamini bado kuna wachezaji hawajapewa nafasi na kutumika kwa kiasi kikubwa na hapo ndipo unapata picha uwepo wa idadi kubwa ya wachezaji lakini pia wasio wa level ya kawaida tu laghasha ni quality ambayo itasaidia timu yao.

Mechi hizi za derby, huwa zinahitaji zaidi wachezaji ambao walikuepo (msimu / misimu nyuma) ambao kwa kiasi fulani tayari wana mwangaza na uelewa wa michezo hiyo.

Hivyo utawaelewa makocha kuweka baadhi ya mali zao mifukoni mwao, na watatumika tu.

Hivyo, huwezi kutoka ukazungumza ukamaliza, juu ya kile ambacho labda ulikiona kwenye michezo yao ya mwanzo, hasa ile ya Ngao, ila as a professional itakutaka kushughudia michezo zaidi.

Tena yenye mnyumbuliko na muingiliano mzuri wa wachezaji wengine pia kwenye kikosi pamoja na ufundi na mbinu sasa za walimu hao, kisha ndiyo unaweza kuzungumza kwa ukubwa zaidi.

Lakini kwasasa tusizungumze sana, tuone na wachezaji wengine ‘hizo mali nyingine za mfukoni’, zikitumika kwanza kisha tutaona sasa mengine. Ila mpaka sasa bado hawana baya, wanayo room kubwa ya kufanya marekebisho & uboreshaji zaidi.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WAWILI YANGA WAPEWA MIKOBA YA CARLINHOS