Habari za michezo

MASHABIKI WAMTAKA PACHA WA AZIZI KI, JE UONGOZI UNASEMAJE!? ISHU IKO HIVI

Staff Desk August 29, 2023 4:13 pm

Saa chache baada ya kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephanie Aiz Ki ‘Master Ki’ alipost kuhusu mchezo wa kwanza wa Ligi ya NBC dhidi ya KMC, na kusema “anamshukuru Mungu kwa kufunga bao na timu yake kupata alama 3.”

Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Wakusanya Ushuru wa Kinondoni huku Wananchi wakitakata kwa kiwango kikubwa hususani Aziz Ki mwenyewe.

Baada ya post hiyo ya Aziz, mchezaji wa RB Salzburg ya Uingereza, Karim Konate alidondosha maoni yake (comment) akionesha kufurahishwa na maendeleo ya swahiba wake huyo ambaye wamewahi kucheza wote ASEC Mimosas kabla ya kila mtu kwenda timu nyingine.

Wananchi na wadau wa soka la Bongo kama unavyowajua, hawakuwa na muda wa kupoteza, Samatta anakumbuka walichokifanya wakati amejiunga na Aston Villa namna walivyokuwa wakitoa maoni yao kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Villa tena kwa Kiswahili.

Tuachane na hilo turudi kwa Aziz Ki. Baada ya Konate kumpongeza Aziz kwa kazi nzuri akiwa na Wananchi, mashabiki wakaamua kushuka nae kwenye uwanja wa comment na kumomba aje kucheza Yanga ili aungane na mshikaji wake huyo

Mmoja wa mashabiki alimkarbisha Konate kwenye chama la mabingwa wa Kihistoria na wa Muda wote wa Tanzania, Yanga. Sasa unawaza, je, Konate kweli anaweza kutoka Rb Salzburg aje kukichafua Tanzania? Kwenye soka lolote linawezekana kama mtonyo upo.

Ikumbukwe kuwa, Konate ndiye alikuwa mfungaji Bora wa MVP wa Ligi Kuu ya Ivory Coast msimu wa mwaka 2021/22 kabla hajaondoka huku akifuatiwa na Aziz Ki kwenye upachikaji mabao.

AZIZ KI AWAGUMZO SOKA LA BONGO, ISHU NZIMA IKO HIVI KAMA WABOVU… NJOONI NYIE! YANGA YAKWEA KILELENI KIBABE,  MAXI KAMA KAWAIDA, MASHABIKI WATAMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply