Habari za Simba leo
Habari za michezo

KRAMO AREJEA MSIMBAZI FULUMZUKA CHEKI BALAA LAKE

Staff Desk August 30, 2023 12:09 pm

Kiungo mshambuliaji Aubin Kramo amerejea mazoezini baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti aliyokuwa ameyepata mazoezini.

Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema nyota huyo ambaye anasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ndani na nje ya Tanzania, ameanza mazoezi ya pamoja na wenzake wote hapo jana Agosti 29, 2023.

“Kila shabiki wa Simba na mashabiki wote wa mpira Afrika wanatamani kumuona mwamba Aubin Kramo akifanya yake uwanjani, taarifa njema ni kwamba yupo fiti na ameanza mazoezi na wenzake baada ya wachezaji kuingia kambini kumuwinda Power Dynamos,” alisema Ahmed.

Mbali na Kramo, Ahmed alisema beki wao katili Henock Inonga naye amerejea rasmi baada ya kupewa mapumziko ya takriban wiki mbili akiunguza majeraha madogo ya bega.

SEPTEMBER 16 SIMBA WANAJAMBO LAO NA POWER DYNAMO…. MAANDALIZI YAPO HIVI GAMONDI: AFUNGUKA KUHUSU WACHEZAJI WAKE KUFUNGA MAGOLI MATANO…. SIO LENGO LETU…AFUNGUKA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply