Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SINGIDA LEO…MASTAA HAWA KUKOSEKANA SIMBA…MBRAZILI ATOA NENO…

KUELEKEA MECHI NA SINGIDA LEO…MASTAA HAWA KUKOSEKANA SIMBA…MBRAZILI ATOA NENO…

Habari za Simba

Kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ngao ya Jamii leo Agosti 10, 2023, Simba SC watawakosa nyota wao wawili, Clatous Chama pampoja na Sadio Kanoute.

Akiuzungumzia maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kocha wa Simba SC, amesema watawakosa nyota hao lakini anao nyota wengine watakaotimiza majukumu vizuri na kupata ushindi.

“Tumejiandaa kwa mchezo huu, tutawakosa nyota wawili lakini haliwezi kutufanya tushindwe kutimiza majukumu yetu ya kusaka pointi tatu,” alisema Robertinho.

Chama anaukosa mchezo huo baada ya kufungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi mwishoni mwa msimu uliopita huku Kanoute akipata kadi nyekundu katika mchezo wa Azam Sports Federation.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA HALI HALISI ILIVYO...ERASTO NYONI NAYE ASHUKURU MASHABIKI SIMBA..."TULIANZA NA TUNAMALIZA WOTE"...