Home Habari za michezo KIBEGI CHA SIMBA CHAINGIZA KIASI HIKI CHA PESA

KIBEGI CHA SIMBA CHAINGIZA KIASI HIKI CHA PESA

Klabu ya Simba imefanya mnada wa KIBEGI kilichokwea kileleni mlima Kilimanjaro pamoja na jezi zilizokuwa na majina ya Viongozi ambao ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na jezi ya Spika wa Bunge, Dkt Tulia Akson.

Katika Mnada huo ambao umefanyika katika Ofisi za Azam TV umezalisha jumla ya Tsh milioni 29, Jezi ya Mo imeuzwa Sh. 2,000,000 kwa Duka la Vifaa la Michezo la Romario Sports ikiwa ni ahadi klabu hiyo iliyoitoa kabla ya kupelewa ilele cha Mlima Kilimanjaro Julai 21.

Jezi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeuzwa kwa Sh. 10,000,000 kwa Benki ya CRDB huku Jezi ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ikiuzwa kwa Sh. 3,000,000 kwenda kwa Sandland Omary ‘Sandland The Only One’

Jezi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi imeuzwa Tsh. 5,000,000 kwa Hasa Clearing and Forwarding huku jezi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ikiuzwa kwa Sh. 4,000,000 kwa S & Sons LTD.

Jezi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Tawi la Simba Makini huku Kibegi kilichokuwa na jezi za klabu hiyo na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kikiuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Saleh Majapa.

SOMA NA HII  BREAKING NEWS: BEKI WA SIMBA CHE MALONE AMEPATA AJALI