Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAMOSI…MASHABIKI YANGA WATAKIWA KUIGA UVAAJI WA MAXI…

KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAMOSI…MASHABIKI YANGA WATAKIWA KUIGA UVAAJI WA MAXI…

Habari za Yanga

Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amewataka mashabiki wote watakaofika uwanjani kesho kutwa kuitazama timu yao itakapokuwa ikicheza na ASAS wafike wakiwa wamechomekea.

Kamwe ametangaza jambo hilo leo Agosti 24, 2023 alipokuwa akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awali Yanga kushinda 2-0.

“Siku ya Jumamosi itakuwa siku ya Maxi Day, lengo ni kuu ni kuhamasisha vijana wetu kwa juhudi zao. Sasa tumeanza na Maxi na wengine watafuta. Hivyo kila shabiki ambaye atafika uwanjani basi afike amechomekea. Ukija na Uzi wako chomekea, ukija na Dira na nguo yoyote ile chomekea…. Tunakwenda Chamazi na muonekano nadhifu tukiwa tumependa kwa kuchomekea”

Katika Hatua nyingine, Alli Kamwe  amesema kesho siku ya Ijumaa Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ atarejea nchini akitokea nchini kwao Afrika Kusini alipokwenda kushughulikia hati yake ya kusafiria (passport) ambayo imejaa.

“Skudu kweli alisafiri kwenda Afrika Kusini na kesho Ijumaa atarejea nchini Kocha Gamondi akitaka kumtumia Jumamosi ni maamuzi yake , amepona kabisa na tuliwaaambia amekwenda kushugulikia passport yake ya kusafiria”

Skudu alishindwa kuendelea na mchezo katika Nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, baada ya kuchezewa rafu dakika ya saba na kiungo wa Azam, James Akaminko.

Na Yanga iliichapa Azam 2-0 mabao yalifungwa na Aziz KI na Clement Mzize ambayo yamefungwa katika dakika 10 za mwisho za mchezo huo.

Skudu ameweka rekodi ndani ya Yanga ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Afrika Kusini kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la Azam.

Mbali na Marumo staa huyo pia amewahi kuzichezea timu za Afrika Kusini, Chippa United na Orlando Pirates kwa mafanikio makubwa, anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu sana kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini.

SOMA NA HII  BAADA YA MAYELE KUSHINDWA KUFUNGA JANA...MSEMAJI WA AZAM KAIBUKA NA HILI....ADAI NI WAKAWAIDA...