Home Habari za michezo MAKOCHA SIMBA, YANGA, AZAM WAKOSA SIFA, TFF YACHUKUA MAAMUZI MAGUMU

MAKOCHA SIMBA, YANGA, AZAM WAKOSA SIFA, TFF YACHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Azam FC Youssouf Dabo ameondolewa kwenye orodha ya Makocha watakaokaa kwenye Mabenchi ya Ufundi wakati wa Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24, ambayo rasmi imeenza leo Agosti 15.

Dabo ambaye alianza kazi rasmi Azam FC wakati wa maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’ ameenguliwa kwenye orodha hiyo, kufuatia kukosa vigezo vya taaluma vinavyotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ na lile la Barani Afrika ‘CAF’.

Kocha mwingine aliyeenguliwa kwenye orodha hiyo ni Kocha Msaidizi wa Simba SC Ouannane Sallami pamoja na Kocha wa Viungo Corneille Hategekimana. Naye Kocha Msaidizi wa Young Africans Moussa Ndaw amepitiwa na panga hilo, sambamba na Kocha Mkuu wa Coastal Union Mwinyi Zahera.

SOMA NA HII  MTOTO HATUMWI DUKANI...FAINALI YA UEFA REAL MADRID vs BORUSSIA DORTMUND