Home Habari za michezo UNAAMBIWA HUYO MAXI NZEGELI YANGA ANAPITA TU….. ISHU IKO HIVI

UNAAMBIWA HUYO MAXI NZEGELI YANGA ANAPITA TU….. ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

Ukiwa unamwangalia Max Nzengeli moja kwa moja kutoka uwanjani [sio kupitia runinga] utagundua anazunguka maeneo yote ya uwanjani, lakini ukitazama mechi kupitia runinga hupati fursa hiyo kwa sababu runinga ni selective.

Ubora na Energy aliyonayo uwanjani umenifanya kufatilia zaidi kujua nini kipo nyuma ya vitu hivyo viwili.

Majibu niliyopewa nataka nikufikishie na wewe ili ujue hakuna mafanikio yanayokuja kwa bahati mbaya! Max anajituma sana nje ya uwanja ili kuwa bora kwenye mechi.

1. Saa moja kabla ya mazoezi ya timu [Yanga], MAX tayari anakuwa uwanjani akifanya mazoezi yake binafsi. Anaomba program kwa mwalimu wa mazoezi na kuifanyia kazi.

2. MAX anafanya sana mazoezi ya kukimbia barabarani [road-work] kwenye mitaa ya Avic Town.

MAX anatambua vizuri kuwa Ligi ya NBC inatupiwa sana macho na mataifa ya Afrika yaliyoendelea kwenye soka [Algeria, Morocco, Misri, Afrika Kusini n.k] kwa hiyo akiuwasha anapandisha thamani yake na kuzivutia klabu zenye msuli wa pesa.

MAX anaitazama Tanzania kama sehemu yake ya kupita kwenda kupiga mpunga mrefu mbele ya safari.

Amekuja Tanzania akiwa hajulikani, ubora anaouonesha uwanjani tayari umeanza kumpa umaarufu na thamani.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU UGAMVI UNAOENDELEA KWENYE KLABU HIYO