Home Habari za michezo UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU SAMIA KUWA MGENI RASMI ISHU IKO HIVI

UONGOZI WA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU SAMIA KUWA MGENI RASMI ISHU IKO HIVI

UONGOZI wa Simba umeeleza sababu ya kumualika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi ni kwa sababu ya ukubwa wa timu hiyo kuelekea siku kubwa ya tamasha lao katika kilele cha siku hiyo.

Tamasha la Simba Day litakalofanyika kesho (Jumapili) na Simba watatumia kutambulisha wachezaji wao wa msimu 2023/24 pamoja na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Power Dynamos ya Zimbabwe, Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally alisema Simba Day ya mwaka huu ni kubwa na maalum na siku kuwa hali iliyopelekea kumuomba Rais Dk. Samia kuwa mgeni rasmi.

Alisema uongozi wa Simba unamshukuru Dk Samia kukubali mwaliko wao na kuwa miongoni mwa watanzania 60,000, watakao hudhuria Simba Day mwaka huu ambayo itakuwa ya aina yake.

“Maandalizi ya Tamasha hili la historia yanaendelea vizuri, kila kiti kipo kwenye mstari huku taratibu zikiwa vizuri na kusubiriwa siku yenye kufika ili madhabiki kupata burudani siku hiyo kuanzania wasanii na mechi mbalimbali za kirafiki ambazo zitacheza timu zote za Simba.

Simba inatimu ya wanawake, vijana na kubwa zote zitapata utambulisho kubwa siku hiyo itatumika kumtambulisha kipa wetu mpya badala ya Mbrazil Jefferson Luis ambaye ni majeruhi,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa kuna mambo makubwa ambayo wanatarajia kuyafanya ndani ya siku hiyo, tayari tiketi za tamasha zimeuzwa zote, wazi mashabiki 60,000 wamethibitisha kuhudhuria Simba Day 2023 ikiwa ni historia mpya kwa kuwa haijawahi kutokea.

SOMA NA HII  MTEGO WA CHAMA DHIDI YA WYDAD UMEKAA HIVI