Habari za Michezo
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA KUSAFIRISHA MASHABIKI….PRIVALDINHO ‘AMLIPUA VIBAYA’ AHMED ALLY…

admin September 9, 2023 8:13 pm

Msimamizi wa Maudhui ya Mitandaoni (Digital Manager) ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Priva Abiudi Shayo ‘Privaldinho’ amemjibu Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ambaye aliyesema Yanga wamemuiga yeye kusafirisha mashabiki nje ya nchi.

“Wanahaha, Mzee Luis Sendeu alisafiri sana na mashabiki na mabasi. Jerry Murro alisafirisha kombe na mashabiki hadi Rwanda (2012).

“Antonio Nugaz alisafiri na mashabiki kwa basi kwenda Ndola (vs Zesco) 2018.

“Mfikirwa na mimi tulienda Dr Congo na mashabiki kwa basi. Huyo nae (Ahmed) kipindi cha nyuma kasafiri sana na mabasi yetu sasa sijui anasema tumeiga nini,” amesema Priva.

WAKATI AL AHLY WAKIICHORA SIMBA KWA ‘DARUBINI’…KAPOMBE KAWACHEKI WEE..KISHA AKASEMA HILI.. WALIOFUNGWA 6-0 NA SIMBA WAKANA KUCHEZA MECHI LEO…ISHU IKO HIVI KUMBE..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply