Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISAAA…YANGA WALIIZIDI SIMBA HAPA KWA JOB….LA SIVYO ANGEKUWA MSIMBAZI …

ZA NDAANI KABISAAA…YANGA WALIIZIDI SIMBA HAPA KWA JOB….LA SIVYO ANGEKUWA MSIMBAZI …

Habari za Yanga

Mchambuzi Clouds FM, Frahan Kihamu amesema kuwa Klabu ya Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili beki, Dickson Job wakati akiwa Mtibwa Sugar lakini walizidiwa ujanja na wapinzani wao Yanga SC.

Job alisajiliwa Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili msimu wa mwaka 2020/21 akitokea Mtibwa ya Morogoro baada ya kuonyesha kiwango bora na Serengeti Boys kisha akasajiliwa na Walima Miwa hao akitokea Moro Kids.

“Dickson Job, Mchezaji ambaye Simba walikuwa wa kwanza kutambua ubora wake na ndio timu ya kwanza kuwasiliana na Mtibwa ili akakipige makutano ya Uhuru na Msimbazi.

“Ni makosa kidogo tu ya kiufundi yalitokea na Kijana akaenda Yanga, kazi nzuri na nzito sana ya Mwenyekiti aliyepita Dr Mshindo Msolla aliyeenda front sana na deal likatimia akaenda Jangwani.

“Moja kati ya Wachezaji ambao siku akistaafu nitaandika visa vyao tukijaaliwa uhai, one of the best,” amesema Frahan Kihamu.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTEMWA SIMBA...GOMES NA ADEL ZRANE WAPATA KAZI YA MAMILIONI...