Home Azam FC DILI LA SHABANI DJUMA NA AZAM …MAMPYA YAIBUKA….

DILI LA SHABANI DJUMA NA AZAM …MAMPYA YAIBUKA….

Habari za Michezo

AZAM FC juzi ilipata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Arta Solar ya Djibouti katika mchezo wa kirafiki ambao kwa mara ya kwanza beki wa zamani wa Yanga, Djuma Shabani aliitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya kukwama kusajiliwa katika dakika za mwisho za dirisha la usajili lililofungwa Agosti 31.

Sasa habari zilizopo ni kwamba, tayari pande zote mbili zimeshakubaliana zikisubiria dirisha dogo, lakini kazi ikiachwa mikononi mwa kocha mkuu Youssouph Dabo ili kumsoma kwa sasa ndani ya kikosi hicho na kuchagua mchezaji gani wa kumchomoa ili beki huyo Mkongomani achukue nafasi kulingana na kanuni.

Kanuni za usajili kwa mapro wa kigeni zinataka klabu isizidishe idadi ya wachezaji 12 na tayari Azam imeshakamilisha, hivyo ili Djuma aingie ni lazima ipunguze mmoja wa nyota waliopo sasa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema suala la usajili wa beki huyo lipo mkononi mwa kocha Dabo.

Popat alisema hawana shaka na kiwango cha nyota huyo ila suala la usajili wake wamemuachia Dabo japo itawalazimu kupunguza wengine ili aingie.

“Tuna wachezaji 12 wa kigeni kama kanuni inavyohitaji sasa endapo kocha ataona anamfaa katika timu basi tutamsajili huku pia suala la kuchagua wa kumpisha tutamuachia atoe uamuzi,” alisema.

Wakati Popat akizungumza hayo, Mwanaspoti linatambua mastaa waliokalia kuti kavu ni kipa Ali Ahamada aliyetakiwa kumpisha Djuma ila aligoma baada ya kudai viongozi walichelewa kumpa taarifa hizo.

Mbali na Ahamada, kipa mwingine Mghana Abdulai Iddrisu huenda pia akaachwa kutokana na kile kinachoelezwa kutokuwa kwenye maelewano mazuri na kocha wake wa makipa, Khalifa Ababakar Fall.

Endapo Iddrisu ataachwa itatoa nafasi kwa kipa Mnigeria, John Noble anayekipiga kikosi cha Kitayosce kusajiliwa kwani viongozi wa timu zote mbili wamewasiliana juu ya upatikanaji wake.

SOMA NA HII  ONANA:- NIMEKOSA ...NIMEKOSA MIMI....NIMEKOSA SANA...MAN UTD KUGUMU...!!!