Home Habari za michezo HIVI NDIVYO MZIMU WA NABI UNAVYOMTESA GAMONDI

HIVI NDIVYO MZIMU WA NABI UNAVYOMTESA GAMONDI

Habari za Yanga leo

Inawezekana mashabiki wa Yanga wanafurahi lakini hakuna mtu mwenye presh kubwa kama Gamondi kwa sababu mtangulizi wake [Nabi] kafanya vitu vikubwa ambavyo Gamondi anapambana kuvifikia.

Nabi ameondoka akiwa amechukua Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC na Azam Sports Federation Cup, yote hayo amechukua mara mbili mfululizo huku akiwa ameifikisha Yanga kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Nabi aliiongoza Yanga kucheza mechi zaidi ya 40 bila kupoteza, kwa hiyo inawezekana vitu ambavyo amevifanya Nabi vikawa vinampa presha kubwa Gamondi. Amendika mchambuzi Edgar Kibwana.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA ISHU YA KAMBI KAMA INAMCHANGANYA...NABI AIBUKA NA MAAMUZI HAYA MAGUMU KWA YANGA...