Home news MINZIRO KAWATAZAMA YANGA WEEE..KISHA AKASHIKA KIDEVU NA KUSEMA HAYA…

MINZIRO KAWATAZAMA YANGA WEEE..KISHA AKASHIKA KIDEVU NA KUSEMA HAYA…


KIKOSI cha Geita Gold kimejifua jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kikijiweka fiti kuwavaa Yanga kesho.

Wakati Yanga ikitua jana jijini hapa, Geita Gold ilifika juzi Alhamisi jioni na jana saa nne asubuhi ikajifua uwanjani hapo kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa kesho Jumapili.

Akizungumza baada ya kuhitimisha mazoezi yao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Kocha wa Geita Gold, Felix Minziro amesema mchezo huo ni mgumu kwao lakini wamejiandaa kushinda.

Minziro amesema wamejiandaa kikamilifu kila idara kwa kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita huku akikazia eneo la ushambuliaji ili kuzitumia vyema nafasi za mabao zinazopatikana kwani katika michezo ya nyuma wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo.

“Tumefanya mazoezi kwa kuangalia idara zote lakini zaidi tumekazia kwenye eneo la finishing (umaliziaji) kwa sababu tumekuwa tukipata nafasi nyingi tunashindwa kuzitumia kwahiyo tunategemea katika mchezo huu tukipata nafasi kama hizo tuzifanyie kazi mwisho wa siku tupate matokeo,” amesema Minziro.

SOMA NA HII  METACHA ATAJWA KIPIGO CHA AZAM...MALALE HAMSINI ASHINDWA KUJIZUIA...AFICHUA SIRI NZIMA...