Home Habari za michezo KILA MCHEZAJI ATAPATA NAFASI YANGA, GAMONDI AFUNGUKA KILA KITU

KILA MCHEZAJI ATAPATA NAFASI YANGA, GAMONDI AFUNGUKA KILA KITU

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema ana wachezaji wengi wazuri katika kikosi chake jambo linalomfanya achukue jukumu la kutoa nafasi kwa kila mmoja kuonesha uwezo wake.

Kauli ya Gamondi imekuja baada ya kuonekana kutumia wachezaji tofauti tofauti katika michuano mbalimbali, huku timu ikicheza kwa kiwango kikubwa bila ya kutetereka na kupata matokeo mazuri.

Kitendo cha kubadili kikosi kinachofanywa na Gamondi, kimekuwa kikiwapa wakati mgumu timu pinzani kushindwa kutabiri wanakutana na timu ya aina gani.

Akizungumzia kuhusu kubadili kikosi mara kwa mara, Gamondi, amesema: “Tuna kundi kubwa la wachezaji wenye ubora mkubwa, wakati mwingine napenda kuwapa nafasi katika michuano tofauti.

“Katika msimu, unaona kunaweza kutokea majeraha, ninachoweza kusema ni kwamba wachezaji wote wanaokaa benchi wanaweza kucheza.

“Wakati mwingine tunahitaji kufanya mabadiliko ya kikosi kwa sababu ya kulinda fitnesi, ninajaribu kutoa nafasi kwa kila mchezaji, najua unafahamu namna ushindani mkubwa ulivyo katika timu, kikubwa ni kupata matokeo mazuri, wakati mwingine huwezi kutoa nafasi hii kwa kila mchezaji, lakini tunajaribu.”

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIJITAFUTA...SIMBA WAZIDI KUTOBOA KIMATAIFA...WAINGIA KWENYE ANGA LA TIMU KUBWA DUNIANI...

1 COMMENT