Home Habari za michezo NAMUNGO KUWAANDALIA SAPRAIZI HII YANGA

NAMUNGO KUWAANDALIA SAPRAIZI HII YANGA

Kocha Mkuu wa Namungo FC, Cedric Kaze amesema licha ya Yanga Sc kuwa kwenye kiwango bora ila yeye kama mkuu wa benchi ya ufundi hawaogopi Yanga.

Kaze ambaye msimu uliopita alikuwa Kocha Msaidizi wa yanga chini ya Nasreddine Nabi, amesema anawajua vizuri Yanga na wao kesho watajitoa wanavyoweza kwenda kupata matokeo ambayo ni bora kwa upande wao.

Kocha huyo raia wa Burundi amesema hayo leo Septemba 19, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa katika Dimba la Azam Complex pale Chamazi, Dar.

“Unajua Yanga Sc wanao timu bora lakini sisi Namungo Fc tumepanga kujitoa leo, maalumu kucheza na Yanga na tumeandaa kitu maalumu kucheza na Yanga Sc.

“Kiukweli hawaaogopi Yanga, kusema kuwa tunahofu bali tutakachoenda kufanya kesho ni kujitoa ili Namungo Fc ipate ushindi,” amesema Kocha Kaze.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:-TUMEPITIA WAKATI MGUMU WIKI MBILI HIZI...TUNAKWENDA KUMFUNGA MTANI....AFUNGUKA HAYA