Home Habari za michezo SIMBA CHAP SANA WAWAHI POWER DYNAMO

SIMBA CHAP SANA WAWAHI POWER DYNAMO

Kikosi cha Simba SC, leo Septemba 27, 2023 kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya kuuzoea uwanja ambao watautumia Jumapili dhidi ya Power Dynamos mchezo wa Klabu Bingwa Afrika.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema hilo leo Septemba 27, 2023 alipokuwa akiuzungumzia mchezo huo.

“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wao wengine hawaujui,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  MECHI HII YA YANGA YAPELEKWA MBELE...HUYO NABI SASA!!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here