Home Habari za michezo AZIZI KI ATOA TAMKO HILI KWA MASHABIKI

AZIZI KI ATOA TAMKO HILI KWA MASHABIKI

Habari za Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Aziz Stephanie Ki amewaita mashabiki wa timu hiyo kujitokeza uwanjani kuwasapoti wachezaji wao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh.

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Jumamosi, Septemba 30, 2023 katika Dimba la Azam Complex baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Rwanda, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-0.

“Kupewa jina langu kwenye mechi hii kubwa ni jambo jema kwangu na kwa kila mmoja, ninapenda kuwaambia Wananchi waje uwanjani kufurahia.

“Huu utakuwa mchezo muhimu sana kwetu kwa hiyo kila mmoja kwa nafasi yake si wachezaji tu hata mashabiki wanapaswa wajae ili kuipa nguvu timu na wachezaji kwa ujumla.

“Kuhusu kufunga siku hiyo naweza kusema kwa mimi jambo muhimu ni timu kwanza. Ukiangalia timu yetu sasa hivi yeyote anaweza kufunga, falsafa yangu sio lazima Aziz Ki afunge, yeyote afunge ili tushinde na mwisho wa siku timu nzima inakuwa na furaha ya ushindi huo.

“Mashabiki waje na funguo siku hiyo kwa sababu siku hiyo itakuwa na Aziz Ki Day na wakati nakuja Yanga kwa mara ya kwanza nilipewa hilo jina la Funguo, kwa hiyo ufunguo tunajua unafungua kila kitu.

“Nawashukuru Wananchi wamekuwa wakijaa Uwanjani kutusapoti na kuhakikisha tunafanya vyema, nawasubiri kuwaona Dimbani,” amesema Aziz Ki.

SOMA NA HII  KOMBE LA SHIRIKISHO: TANZANIA PRISONS 0-0 YANGA