Home Habari za michezo BALEKE ATOA AAHADI HII JE ATATOBOA

BALEKE ATOA AAHADI HII JE ATATOBOA

Mshambuliaji wa Simba, Mkongomani, Jeane Baleke, ameahidi kuendelea kufunga mabao katika kila mchezo ili afanikishe malengo yake ya kufikisha mabao zaidi ya 20 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu na kuwa mfungaji bora.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita, tangu apige hat trick katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza nasi, Baleke mwenye mabao matano katika Ligi Kuu Bara msimu huu, alisema msimu uliopita alishindwa kufikisha idadi hiyo ya mabao, kutokana na kujiunga na timu katikati ya msimu.

Baleke alisema anaamini malengo yake yatafanikiwa ya kuchukua ufungaji bora, kama akiendelea kupata ushirikiano kutoka kwa wenzake na asipopata majeraha.

Aliongeza kuwa, licha ya ugumu wa ligi uliokuwepo, lakini hiyo haimfanyi ahofie malengo yake kutotimia msimu huu, atahakikisha anatumia vema kila nafasi atakayoipata.

“Binafsi natamani kuona nikifunga mabao kuanzia 20 kwenye ligi msimu huu, huku nikiamini yatatosha kuisaidia Simba kutwaa ubingwa.

“Nafahamu ugumu wa ligi ambao tayari nimeuzoea kwa miezi sita niliokuwepo hapa Simba, hivyo nimejipanga vema kupambana na timu yoyote nitakayokutana nayo katika ligi,” alisema Baleke.

SOMA NA HII  MASHUSHUSHU WA YANGA...WAPATA TAARIFA HIZI NYETI ZA RIVERS...KUMBE WANA MBINU HIZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here