Home Habari za michezo AZIZI KI AFUNGUKA KILICHOMFELISHA MSIMU ULIOPITA,….. SASA MAMBO NI HIVI

AZIZI KI AFUNGUKA KILICHOMFELISHA MSIMU ULIOPITA,….. SASA MAMBO NI HIVI

Habari za Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Aziz Stephanie Ki amesema kuwa kilichomfanya asifanye vizuri msimu uliopita ilikuwa ni ugumu wa kuzoea mazingira mapya ya Tanzania baada ya kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Msimu uliopita Aziz Ki alihusika katika mabao 13 ya Yanga kwenye Ligi Kuu ya NBC akifunga mabao 9 na kutoa assits 4. Msimu huu mpaka sasa akihusika kwenye mabao 3, amefunga mabao mawili na assist moja katika michezo mitatu ya Ligi.

“Siri ya mimi kuendelea kufanya vizuri msimu huu ni Mungu, sababu haya ni maisha na huwezi kuwa juu siku zote, kuna wakati unakuwa na siku mbaya hivyo unatakiwa kumshukuru Mungu na kusema asante kwa kila jambo.

“Unajua wakati unapohama Ligi moja kwenda nyingine kwa mara ya kwanza inakuwa ngumu kwa sababu unatakiwa ujifunze baadhi ya vitu, uzoee mazingira na hali ya maeneo husika.

“Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwa sababu kulikuwa na nyakati nzuri na mbaya, huzuni na furaha, kwa hiyo nilijifunza soka la Tanzania na sasa nimezoea. Nina marafiki na pia tuna timu nzuri kila mmoja anajitoa, hivyo ni wakati wangu wa kufurahia soka,” amesema Aziz Ki.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATAMBA KUHUSU KIKOSI CHA SIMBA

1 COMMENT

  1. Hakika umenena Vyema Kikubwa endeleeni kujituma na kuipambania team huku Ukizingatia kuwa hakuna Mafanikio bila Mungu na nidhamu pia