Home Uncategorized IHEFU FC WANAJAMBO LAO NDANI YA LIGI KUU BARA

IHEFU FC WANAJAMBO LAO NDANI YA LIGI KUU BARA


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC amesema kuwa wachezaji wake wapo vizuri ndani ya uwanja ila wanakosa uzoefu katika kutafuta matokeo jambo ambalo limekuwa likiwapa shida ila anaamini atalifanyia kazi.


Ndani ya msimu wa 2020/21 ikiwa imecheza jumla la mechi 15 imeshinda mbili ambapo ya kwanza ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na jana ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar ukiwa ni mshindi mkubwa kwao.

Joseph Kinyozi alikuwa wa kwanza kufunga Uwanja wa Sokoine dakika ya 38 na kuwafanya waende mapumziko wakiongoza kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili Kagera Sugar waliwasha moto na kuweka usawa kupitia kwa Sadat Mohamed dakika ya 60. Shukran kwa Issa Ngoah wa Ihefu ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 54.

Ushindi huo unaifanya Ihefu kupanda nafasi moja kutoka ya 18 mpaka ya 17 ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 15 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 11 na pointi 18.

Katwila amesema bado wataeendela kupambana kutimiza jambo lao ambalo ni kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  TOTTENHAM WABISHI KWELI, WAIGOMEA MKWANJA WA INTER MILAN NA KUWAPA MASHARTI MENGINE