Home Habari za michezo “WANACHAMA LIPENI ADA TUMALIZE MADENI” – YANGA

“WANACHAMA LIPENI ADA TUMALIZE MADENI” – YANGA

Habari za Yanga SC

Baada ya moja ya Mashabiki wa Yanga SC kuhoji kuhusu kesi za madai pamoja na kufungiwa na FIFA kufanya usajili ambazo zimekuwa zikiiandama klabu yake siku za hivi karibuni, mwanasheria wa timu hiyo Patrick Simon amemjibu Shabiki huyo kuhusu sababu za madeni na kesi hizo

Shabiki huyo @mvemb_a aliuliza hivi; “Binafsi naumizwa na hizi kesi za kila siku na kufungiwa hakuna hata kesi tumeshinda na wewe upo wakili unaetambulika na FIFA hii kila siku kulipa inatokana na nini mkuu.”

Mwansheria wa Yanga Simon Patrick amemjibu shabiki huyo kwa kuandika; “Klabu imekuwa ikinitahidi kulipa madeni yote ya zamani na ya sasa, kwa hiyo mpaka pale yatakapomalizika kushtakiwa ni jambo la kawaida, hamasisha wanachama walipe ada zao na klabu imalizane na madeni uje uone kama kutakuwa na kesi tena.”

Yanga bado wapo kwenye mgogoro na aliyekuwa mchezaji wao, Gael Bigirimana raia wa Burundi ambaye amewashtaki FIFA na kusababisha timu hiyo kufungiwa kusajili mpaka pale watakapomaliza kumlipa.

Habari za yanga

Aidha, katika post yake, Patrick alisema amewaombea ulinzi na afya njema ili muendelee kuona show za Maxi, Mudathir, Yao, Nondo, Job, Pacome, Kibwana (Mtu mshoti), Dr. Aucho, Mkude na Farid na wachezaji wengine.

“Nawaomba mashabiki tuanze kujiandaa kwa safari ya Kigali – Rwanda, utaratibu utatolewa ili tukaishangilie timu yetu kwenye mchezo wetu dhidi ya Al Merrikh, utakaochezwa tarehe 16/09/2023,” amesema Wakili Patrick.

SOMA NA HII  YANGA SASA NI CHUMA BAADA YA CHUMA, WAMTAMBULISHA MCHEZAJI WAO MPYA SIO POA