Habari za michezo

SHABIKI WA YANGA ALIYEPOKEA KIPIGO NA MASHABIKI WA SIMBA AFUNGUKA TUKIO ZIMA HAPA

Staff Desk October 31, 2023 5:47 pm

Jumamosi ya Oktoba 28 Timu ya Simba ilikuwa wenyeji wa Ihefu katika Uwanja wa Mkapa mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo uliokuwa na vuta nikuvute ulimalizika kwa Simba kuondoka na alama 3 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo ule kuliibuka tukio la Mashabiki wa Simba kuonekana wakimshambulia shabiki alionekana amevaa jezi ya Yanga.

Sasa Shabiki huyo kuputia kituo cha Efm amefunguka sababu za kupokea kichapo ambapo amesema;

“Sababu za mashabiki wa Simba kunipiga ni kuhisi imani za kishirikina, wao walikuwa wanasema kuwa mimi ndio chanzo cha kuzuia Simba Wasishinde katika Mchezo huo, kitu ambacho sio cha kweli,”

KUELEKEA DABI YA KARIAKOO MASTAA HAWA SIMBA SASA NI MTEGO AZIZ KI AFUNGUKA KUHUSU DABI YA KARIAKOO……. AIHAKIKISHIA YANGA USHINDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply