Home Azam FC AZAM NA SIMBA MAJI YA SHINGO

AZAM NA SIMBA MAJI YA SHINGO

Habari za Simba SC

Hadi sasa wanachokifanya Yanga Sc tangu kuanza kwa msimu huu wa mashindano mbalimbali unaweza ukaona kama ni bahati kwa jicho la kishabiki ila kiuhalisia hapana ni ubora walionao.

Tangu katika ile michuano midogo ya Ngao ya Jamii pale Jijini Tanga ni kwamba Yanga tayari walishaonyesha wana kikosi ambacho kina ushindani kuliko Simba, Azam FC na klabu nyingine.

Angalia katika mechi zao 6 za mashindano mbalimbali wamefunga magoli 13 na kufungwa goli moja pekee, kitu ambacho Azam FC na Simba hawajaweza kukifanya. Hii ndio Yanga

Kama ukikaa alafu ukawa unasema hiki ambacho wanakifanya Yanga ni bahati basi utakuwa unaukosea heshima mpira wa miguu. Kwa sasa Yanga wanatafuta kuweka standard yao katika michuano ya Kimataifa.

SOMA NA HII  SENZO - YANGA HATURUDI NYUMA...AFUNGUKA VIKWAZO VILIVYOPO...BUMBULI AACHIA TABASAMU...