Home Habari za michezo AFCON 2027….KENYA KUJENGA UWANJA WA FAINAL….CAF KUIMWAGIA NEEMA ZAIDI…

AFCON 2027….KENYA KUJENGA UWANJA WA FAINAL….CAF KUIMWAGIA NEEMA ZAIDI…

Habari za Michezo

Serikali ya nchini Kenya ipo kwenye mpango wa ujenzi wa Uwanja mpya utakaoitwa TALANTA SPORT CITY utakaokuwa na uwezo wa kuchukuwa watazamaji 60,000,

Malengo yao makubwa ni kuhakikisha kuwa wanapata nafasi ya kuweza kuandaa mchezo wa fainali katika AFCON ya 2027 baada ya kuona nafasi ni kubwa kwa Tanzania kutokana na uwepo wa Uwanja wa Benjamin Mkapa unaobeba watazamaji 60,000.

Katika hatua nyingine,Imefahamika kuwa Taifa la Kenya ndio litakuwa mwenyeji wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024.

Bado shirikisho la soka barani Afrika CAF hawajathibitisha taarifa hiyo lakini taarifa kutoka vyanzo kadhaa nchini Kenya vimeripoti uwezekano wa michuano hiyo kuchezwa nchini humo.

Mara kadhaa Kenya wamekuwa na bahati ya kushinda nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano kadhaa lakini wanaishia kupokwa nafasi kwasababu ya miundombinu ya viwanja.

Ikumbukwe mwaka 2018 walipata nafasi kama hiyo lakini walishindwa kutokana na ukosefu wa miundombimu rafiki.

Aidha Kenya ni muandaaji mwenza wa AFCON 2027 pamoja na Tanzania na Uganda.

SOMA NA HII  YANGA WAONYESHWA MWANGAZA WA USHINDI RWANDA