Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA AZAM FC…GAMONDI ALIANZISHA UPYA KWA MASTAA WA YANGA…

KUELEKEA MECHI NA AZAM FC…GAMONDI ALIANZISHA UPYA KWA MASTAA WA YANGA…

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewabadilishia programu wachezaji wake kulingana na ubora wa Azam FC ambao watakutana nao katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 22, mwaka huu, Yanga watakuwa wenyeji wakiwakaribisha Azam FC , uwanja wa Azam,Chamazi Dar-es-Salaam.

Kocha Gamondi alisema licha ya kutokamilika kwa wachezaji wote ameanza mazoezi ya nguvu na nyota waliopo wanakuwa imara kila upande.

Alisema anatambua ubora wa Azam FC lakini hawatokubali kupoteza mchezo huo ambao utakuwa wa ushindani mkubwa kwa sababi ya kila mmoja anahitaji alama muhimu.

β€œKila mchezaji anatambua wajibu wake, tupo vizuri kila nafasi na tunaendelea kuwa imara katika sehemu chache ikiwemo ulinzi na ushambuliaji ambazo zilikuwa na kasoro.

“Kikubwa tunataka ushindi wa mbao mengi mbele ya Azam FC, naamini hata wapinzani wanafanya maandalizi, kwetu tunahitaji kuingia kwa mbinu tofauti na michezo iliyopita kwa sababu tunahitaji kutetea taji,” alisema kocha huyo.

Aliongeza kuwa hawatoruhusu kupoteza mchezo wa pili kwenye ligi ikiwa mbichi ndio wakati wa kutafuta matokeo mazuri katika kila mechi zilizopo mbele yao bila ya kujali wanacheza ugenini au nyumbani.

Gamondi alisema kila mechi inekuwa na maandalizi yake na kuelekea mchezo huo wanajiandaa kulingana na ubora wa Azam FC ambao wamekuwa nao kwa sasa.

SOMA NA HII  BAADA YA MIAKA MINGI KUPITA..KOTEI AFICHUA KILICHOMUONDOA SIMBA...AMTAJA HERSI WA YANGA...