Home Habari za michezo ISHU YA KUANZIA BENCHI KILA MECHI ZA YANGA YAMUIBUA SKUDU…AFUNGUKA YA MOYONI…

ISHU YA KUANZIA BENCHI KILA MECHI ZA YANGA YAMUIBUA SKUDU…AFUNGUKA YA MOYONI…

Habari za Yanga SC

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Afrika Kusini Skudu Makudubela, ameweka wazi kuwa, hana tatizo lolote na Benchi la ufundi la Young Africans linaloongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi.

Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya Young Africans akitokea Marumo Gallants ya kwao Afrika Kusini, hajawa na nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba uliopo ndani ya timu hiyo.

Mbali na ushindani, pia alianza msimu akipambania hali yake baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga alipopata maumivu ya mguu dakika ya sita alipochezewa faulo na James Akamiko.

Nyota huyo amesema: “Nipo Young Africans na nifurahi kuona tunapata matokeo mazuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza, hilo ni jambo la msingi.

“Kutokucheza ama kucheza hilo halinipi shida kwani kuna wachezaji wengi ndani ya Young Africans.

“Wanapofunga kwenye mechi zetu wale wanaopewa nafasi hii inatupa nguvu sisi kwa ajili ya kuendelea kupambania malengo yetu. Kuhusu nani aanze kwenye mchezo husika huo ni mpango wa benchi la ufundi na hatuna matatizo nao kabisa.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA TAARIFA ZAKE ZA KUWA MAJERUHI ZIPO NYINGI..CHICO AIBUKA NA KUVUNJA UKIMYA..