Home Habari za michezo KWELI HII HATARI WATU WANAIJUA SIMBA KULIKO STARS

KWELI HII HATARI WATU WANAIJUA SIMBA KULIKO STARS

Habari za Simba SC

Mchambuzi wa soka Bongo, Amri Kiemba amechambua kuhusu mashabiki wa soka kuizungumzia klabu ya Simba kuliko timu ya Taifa.

Huu hapa uchambuzi wake;

“Inawezekana TFF ina lengo zuri la kuifanya Taifa Stars kuwa mbali na vyombo vya habari pamoja na mashabiki wa soka lakini kuna siku watawahitaji watu uwanjani na hapo TFF italazimika kutumia nguvu nyingi kuwashawishi.

Mwaka 2027 tutakuwa wenyeji wa AFCON, tunahitaji watu. Kama watu hawapo nyuma ya timu yao muda wote ikifika wakati wa AFCON ndio tuanze kuhimizana kwenda uwanjani kwa sababu sisi ndio wenyeji tutakuwa tumechelewa.

Kwa sasa watu wanafahamu sana kuhusu mechi ya Simba vs Al Ahly [African Football League] ambayo itachezwa Ijumaa lakini hawajui kitu kuhusu mechi ya Taifa Stars ambayo imechezwa jana!”

Ile mijadala ya kwa nini fulani ameitwa halafu fulani hajaitwa ndio inaongeza ufuatiliaji wa timu ya Taifa. Kila kitu kina chanya na hasi, hata hii kuita timu hadi inacheza kimyakimya nayo ina hasi na chanya.

SOMA NA HII  DILUNGA ATAJA SABABU YA KUTUSUA SIMBA