Home Uncategorized ZAHERA AFUNGUKA JUU YA AJIBU KUSAINI SIMBA

ZAHERA AFUNGUKA JUU YA AJIBU KUSAINI SIMBA


Kocha Mkuu wa Yanga, Emmanuel Amunike amesema kuwa inawezekana Ibrahim Ajibu aliogopa kujiunga na TP Mazembe ya Congo ndiyo maana alikataa kusajiliwa.

Zahera ambaye hivi sasa anatarajiwa kutua nchini baada ya timu yake ya Taifa ya Congo kutolewa kwenye michuano ya AFCON huko Misri, ameeleza hayo kufuatia mchezaji huyo kusaini Simba.

Kocha huyo mwenye maneno mengi amefunguka kuwa hawezi kumuelezea kwa mengi Ajibu lakini akifunguka kwa kusema aliogopa kujiunga na Mazembe.

Ameongeza kwa kusema kuwa aliogopa sababu ya fedha ikielezwa kuwa dau walilotaja Mazembe lilikuwa dogo kwake.

Mbali na hilo, Zahera pia ameeleza suala la Ajibu kusaini Simba yeye kwake halina tatizo akisema kuna wachezaji wengine wengi tu ambao wanamudu nafasi yake Yanga.

Ajibu tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba ambayo alikuwa nayo kabla ya kwenda Yanga misimu miwili iliyopita.

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WAANZA NA HUYU