Home Habari za michezo LICHA YA SIMBA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI ROBERTINHO AWAJIA JUU WACHEZAJI

LICHA YA SIMBA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI ROBERTINHO AWAJIA JUU WACHEZAJI

Habari za Simba

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa Simba wanatinga hatua ya makundi wakiwa hawana furaha mashabiki, huku Kocha Mkuu, Roberto Oliveira akiweka wazi kuwa umakini kwenye umaliziaji nafasi uliwaponza.
Simba wanatinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-3 faida ya mabao ya ugenini kwa kuwa mchezo wa kwanza ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba.
Mabao yote ya ugenini yalifungwa na kiungo Clatous Chama raia wa Zambia.
Kwenye mchezo wa pili wa marudio uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Oktoba Mosi kipindi cha kwanza walichezawachezaji wa Simba walicheza chini ya kiwango huku wakishindwa kuwa na maelewano mazuri.
Kipindi cha pili baada ya kurejea kutoka kwenye vyuma vya mazungumzo angalau kulikuwa na mabadiliko kidogo kwenye kutafuta bao pamoja na mipango kazi ya wachezaji.
Bao la mapema la Power Dynamos kupitia kwa Andy Boyel liliwapa tabu Simba dakika 45 za mwanzo kwa kuwa walifungwa dakika ya 16 huku safu ya ulinzi ikiwa haina namna kuzuia.

Kuingia kwa nahodha John Bocco kuliongeza presha eneo la ushambuliaji mpaka kupatikana kwa bao ambalo nyota wa Power Dynamos Kondwan Chidon alijifunga dakika ya 69.

Simba inaungana na Yanga katika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni rekodi kubwa kwa timu mbili kutoka Tanzania kuwa kwenye hatua ya makundi.
Upande wa mipango ni muhimu Simba kufanya maboresho makubwa kuanzia safu ya ushambuliaji na viungo ambao wanaoneana kucheza kwa uwezo binafsi na sio timu.

SOMA NA HII  KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA....GEITA GOLD WAPEWA MIFUPA MIGUMU TUPU...AZAM WAPEWA WAARABU WEUSI TUPU...