Home Habari za michezo FT: SIMBA 2-2 AL AHLY……WAARABU WABANA KILA KONA….GAMONDI NA YANGA YAKE NDANI…

FT: SIMBA 2-2 AL AHLY……WAARABU WABANA KILA KONA….GAMONDI NA YANGA YAKE NDANI…

FT:SIMBA 2-2 AL AHLY

SIMBA SC imeshindwa kutamba katika uwanja wke wa nyumbani baada ya kufungana mabao 2-2 na Al Ahly ya Misri mchezo wa robo Fainali ya Michuano Mipya ya African Football League ambayo imezinduliwa leo katika Uwanja wa Benjamini Mkapa,jijini Dar Es Salaam.

Wageni walienda mapumziko wakiwa wanaongoza bao moja lililofungw na Reda Slim dakika ya 45 + 1 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Simba SC.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko ya haraka haraka na kuendelea kuishambulia ngome ya Al Ahly ambao walikuwa wanacheza kwa kushambulia na kuzuia.

Simba walicharuka na kupata mabao mawili ndani ya dakika ya saba yakifungwa na Kibu Denis dakika ya 53 kwa pasi ya Clatous Chama,bao la pili likifungwa kwa kichwa na Saido Kanoute dakika ya 59.

RAIS MWINYI, GAMONDI NDANI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi ameambatana na viongozi mbalinbali katika mchezo huo wa ufunguzi wa michuano ya Afrika Football League.

Michuano hiyo iliyozinduliwa rasmi leo ikiwa mara ya kwanza kuanzishwa huku Simba wakiwa wenyeji wakiwakaribisha Al Ahly.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ulihudhuluwa na vongozi wengine wa mpira wa miguu kutoka mashirikisho mbalimbali akiwemo Rais wa Shirikisho la Soka ulimwenguni (Fifa) Gianni Infantino ambaye aliwasalimia wanasimba kwa kauli mbiu ya “Simba Nguvu Moja”.

“Leo Simba dhidi ya Al Ahly mpira wa miguu umekuwa ukiunganisha dunia, leo unaunganisha kutoka hapa Tanzania, furahieni michuano ya Afrika Football League,” alisema Infantino baada ya ufunguzi wa mashindano hayo.

Naye Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ni miongoni mwa mashuhuda wa mchezo huo, aliingia uwanjani saa 11:21 jioni na kukaa jukwaani kwa lengo la kuangalia mchezo huo mahususi kuwasoma Al Ahly ambao wako kundi mmoja ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya timu kumaliza kufanya mazoezi ya kupasha misuli moja na kwenda vyumbani kwa ajili ya kujiandaa na mchezo, kulikuwa na burudani ya muziki akiwemo Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Saleh (Ali Kiba).

Mashabiki wa Simba walijitokeza kwa wingi hawajamuangusha Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya timu hiyo, Ahmed Ally ambaye alitumia siku saba kufanya hamasa ya kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.

SOMA NA HII  HIKI HAPA NDIO KILICHOMPONZA ROBERTINHO MBELE YA AL AHLY