Home Uncategorized ARSENAL YAMTAKA KIUNGO WA SEVILLA

ARSENAL YAMTAKA KIUNGO WA SEVILLA


IMEELEZWA kuwa mabosi wa Klabu ya Arsenal wanahitaji saini ya nyota wa Klabu ya Sevilla, Joan Jordan ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Jicho la Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta linatajwa kuitazama kwa ukaribu saini ya nyota huyo mwenye miaka 26 raia wa Hispania.

Ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye London Dabi walioupata Desemba 26 umemfanya Arteta afikirie kuongeza nguvu eneo la kiungo ili kupata ushindi zaidi kwenye mechi zake.

Arteta ana matumaini kwamba akipata saini ya nyota huyo ataongeza nguvu ya kujiamini kwa kikosi chake kwa kuwa ana uwezo pia wa kufunga kwa kuwa ndani ya La Liga akiwa amecheza jumla ya mechi 41 amefunga mabao mawili.

Arsenal ipo tayari kuweka dau la pauni milioni 32 ili kumpata nyota huyo ambaye amewahi kucheza pia ndani ya Klabu ya Eibar msimu wa 2017-19 na alicheza jumla ya mechi 71 na kufunga mabao 10.


SOMA NA HII  MASHINE YA KAZI SIMBA YAUNGANISHWA KWENYE KIKOSI, RUKSA KUWAVAA COASTAL UNION