Home Uncategorized SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU JONAS MKUDE

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU JONAS MKUDE

 


KOCHA wa zamani wa Klabu ya Simba, Jamhuri Khwelu maarufu kama Julio amesema kuwa suala la nidhamu kwa mchezaji ni jambo la msingi.


Maneno hayo ameyasema ikiwa ni baada ya kiungo wa Simba, Jonas Mkude kusimamishwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.


Mkude amesimamishwa kwa muda kupisha uchunguzi wa tuhuma ambazo anatajwa kukutwa nazo za utomvu wa nidhamu.

“Nidhamu ni jambo la msingi kwa kila mchezaji hivyo ni ngumu kwa mafanikio ndani na nje ya uwanja kupatikana hivyo kwa walichokifanya Simba naona ni sawa japo ni maamuzi magumu,” . 

SOMA NA HII  YANGA YATUMA SALAMU ZA POLE KWA SIMBA DHIDI YA AL AHLY