Home Habari za michezo SHABIKI WA YANGA ALIYEPOKEA KIPIGO NA MASHABIKI WA SIMBA AFUNGUKA TUKIO ZIMA...

SHABIKI WA YANGA ALIYEPOKEA KIPIGO NA MASHABIKI WA SIMBA AFUNGUKA TUKIO ZIMA HAPA

Jumamosi ya Oktoba 28 Timu ya Simba ilikuwa wenyeji wa Ihefu katika Uwanja wa Mkapa mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo uliokuwa na vuta nikuvute ulimalizika kwa Simba kuondoka na alama 3 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo ule kuliibuka tukio la Mashabiki wa Simba kuonekana wakimshambulia shabiki alionekana amevaa jezi ya Yanga.

Sasa Shabiki huyo kuputia kituo cha Efm amefunguka sababu za kupokea kichapo ambapo amesema;

“Sababu za mashabiki wa Simba kunipiga ni kuhisi imani za kishirikina, wao walikuwa wanasema kuwa mimi ndio chanzo cha kuzuia Simba Wasishinde katika Mchezo huo, kitu ambacho sio cha kweli,”

SOMA NA HII  MASHABIKI WA YANGA KIGALI WAPATA ZALI HILI