Home Habari za michezo SIMBA WAOGA MINOTI KUTOKA CAF ISHU IKO HIVI

SIMBA WAOGA MINOTI KUTOKA CAF ISHU IKO HIVI

Jezi mpya za Simba leo

Simba SC jana ilicheza mechi ya kirafiki ya kujiandaa na pambano la michuano mipya ya African Football League (AFL) kwa kuikandika Dar City mabao 5-1, huku kipa Aishi Manula akicheza kwa mara ya kwanza kwa dakika 40 tangu arejee kutoka majeraha, lakini klabu hiyo ikiwa na jeuri ya fedha za CAF.

Simba inajiandaa dhidi ya Al Ahly ya Misri, kwenye uzinduzi wa michuano hiyo mipya Ijumaa ya Oktoka 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kwenda kurudiana siku nne baadaye Cairo, Misri na mshindi wa jumla ataingia nusu fainali.

Kwenye Uwanja wa Mo Arena, Bunju Simba dhidi ya Dar City mabao mawili yalifungwa na Shaaban Idd Chilunda, Saido Ntibazonkiza, Luis Miquissone na Willy Onana kila mmoja akifunga moja moja na kushuhudiwa Manula akirudi uwanjani tangu alipoumia Aprili 7 mwaka huu kabla ya kutolewa na kumpisha kipa mpya, Hussein Abel.

Achana na mechi hiyo ambalo Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ametumia kuliweka fedha jeshi lake, lakini Wekundu hao kuna utamu wa mkwanja mrefu wanakunja ambao utawapa jeuri kubwa.

Simba kabla ya kushuka uwanjani kuikabili Al Ahly ya Misri kwenye mchezo huo tayari Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeshaipa mkwanja wa maana usiopungua Dola 400,000 (Sh 1 bilioni).

Simba imelazimika kuchukua fedha hizo baada ya CAF kupunguza kutoka viwango vya awali ambapo ilikuwa kila timu inayoshiriki katika hatua hiyo ya robo fainali ilikuwa ivune Dola 1 milioni (zaidi ya Sh 2.5 bilioni) kabla ya kupunguzwa na kuwa hizi Sh 1 bilioni kwa mujibu wa viongozi wa Simba.

Simba imesema hakuna shida wakapiga hesabu ndefu na kupeleka mzigo huo kwa mastaa wao kuhakikisha wanafanya kweli kwa kuichapa Al Ahly huku pia wakitumia mzigo huo kuigharamia timu hiyo kwenye mchezo wa marudiano.

Mabosi wa Simba wamepanga kutumia fedha hizo kiasi kikubwa kwa wachezaji wao, lakini hesabu zao wakitaka timu yao iwapeleke hatua ya nusu fainali ambayo watavizia kiasi cha 2.2 bilioni endapo watatinga hatua hiyo kwa kuwaondoa Ahly.

Awali bingwa wa michuano hiyo ilikuwa anazoa Dola 4 milioni (zaidi ya Sh 10 bilioni), huku wa pili atazoa Dola 3 milioni (zaidi ya Sh 7.5 bilioni) wakati timu itakayiotinga nusu fainali itakomba Dola 1.7 milioni ( zaidi ya Sh 4.3 bilioni), hata hivyo kuna mabadiliko yamefanyika kimyakimya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Try Again amesema klabu yao inataka kutumia fedha hizo kuwapa morali wachezaji wao kufanya vizuri wakitamani kutinga nusu fainali kwanza kablam ye hesabu nyingine.

Try again alisema ingawa bodi yao inaridhishwa na maandalizi yao ya kikosi hicho, lakini wasiwasi wao ni kurejea kwa mastaa waliokuwa timu za taifa ambao maombi ya kuwazuia yameshindwa kusikilizwa kwa kupumzishwa kwenye ratiba za mechi hizo za kirafiki za timu za taifa.

“Ni kweli kuna hilo suala la hizo fedha watu wafahamu kwamba hivyo viwango kwanza vimebadilishwa, nadhani CAF watatangaza baadaye, lakini sisi Simba tunalijua hilo,” alisema Try Again ambaye amehusika kusimamia kuundwa kwa kikosi hicho ambacho hakijapoteza hata mchezo mmoja msimu huu.

Try Again alisema: “Tunaridhishwa na maendeleo ya kikosi chetu makocha na wachezaji waliobaki wanaendelea na maandalizi na sisi viongozi tunasimamia mambo ya kitawala dua zetu ni kwa wachezaji wetu waliopo timu za taifa warudi salama.

“Tunakabiliwa na changamoto tukisubiri kuona watarejea lini na watapataje muda wa kutosha wa maandalizi ya pamoja na wenzao.

“Tuliwasilisha maombi kwa wenzetu lakini yameshindwa kupewa uzito, haya hayakuwa maombi tu ya viongozi yalikuwa ni maombi ya makocha ambao walidhani yangesikilizwa kulingana na ugumu wa mechi ambazo zinakuja mbele yetu.”

Mbali na fedha za African Football League, Simba imejihakikishia pia kuvuna kiasi cha Dola 700,000 (karibu Sh 1.8 bilioni) kwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyo pia kwa Yanga iliyofuzu hatua hiyo baada ya miaka 25 iliyopita.

SOMA NA HII  KUMBUKIZI HIZI ZA DABI YA WATANI WA JADI...ZAIBEBA SIMBA WAZI WAZI